Rais Jakaya Kikwete, akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan.
Baadhi ya waandishi na wapiga picha wa vyombo vya habari mbalimbali wakiwajibika uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete, akiingia uwanjani kwa kutumia gari la wazi wakati akiwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuapishwa.
Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhan.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Ngao na Mkuki, aliokabidhiwa na wazee, ikiwa ni ishara ya kujilinda na maadui mara baada ya zoezi la kuapishwa.
Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride maalum baada ya kuapishwa.
Hata mapaparazi nao walikuwa bize huku na huko ili kuhakikisha wananasa picha zote zinazohusu sherehe hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa, Viongozi, Ndugu na Jamaa wa Waheshimiwa wakiwa jukwaani kuhudhulia sherehe hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Kingunge Ngombalemwilu na wazee wengine maarufu wa CCM, baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa.
Anne Kilango, akimnong’oneza jambo mumewe, Malechela, wakiwa jukwaani .





No comments:
Post a Comment