Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AANZA KAZI RASMI IKULU LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu baada ya kuwasili kwenye Ofisi yake kuanza kazi rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi Makamu wa Rais (Mazingira), wakati alipofika ofisini hapo kusaini kwa mara ya kwanza na kuanza kazi rasmi leo.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akielekezwa jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ruth Mollel, wakati alipokuwa akimuonyesha jengo jipya la Ofisi ya Makamu wa Rais linaloendelea kujengwa wakati Makamu wa rais alipofika kuripoti ofisini leo. (
Makamu wa Rais akiongozana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa rais, Bi. Ruth Mollel, wakati alipofika kuanza kazi na kukagua baadhi ya maeneo ya ofisi hiyo leo.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.