Habari za Punde

*HAPPY BIRTHDAY JACQUELINE, HONGERA KWA KUWAKUMBUKA YATIMA

Hongera Mrembo Jacqueline kwa kutimiza miaka 25 sasa tangu kuzaliwa kwako mungu akuzidishie heri na uzima na moyo wa kuwakumbuka Yatima kama hivi. Na hii ndiyo Keki ya mrembo huyo inayosubiri kukatwa rasmi leo jioni.
Jacqueline, akipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya Watotot yatima wa Kituo cha New Life Orphans Home, wakati alipowatembelea watoto hao na kucheza nao na kufurahi kwa pamoja, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku yake ya kuzaliwa.
Ilikuwa ni furaha kwa watoto hao na mrembo huyo mpenda watoto, kwani baby huyu aliyebebwa hakutaka hata kushuka wakati alipokuwa akiwaaga kuondoka mahala hapo kwa jinsi alivyojihisi furaha kwa wakati huo, ama hakika ilikuwa kazi kubwa kumwacha mtoto huyu na kuondoka.
Hapa akimfuta uchafu puani mtoto huyo wakati akisubiri kuombewa dua na watoto hao.
Jacqueline na rafiki zake wakimsikiliza kwa makini Mama mlezi wa Kituo hicho wakati akiwapa angalau kwa ufupi Historia ya kituo hicho.
Jacqueline akipiga picha ya kumbukumbu na rafiki zake pamoja na Mama mlezi wa Kituo hicho (kulia) baada ya kumaliza zoezi la kuchati na watoto hao na kuwagawia zawadi. HAPPY BIRTHDAY BABY J

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.