Habari za Punde

*MDAU KUTOA NI MOYO CHANGIA KUSAIDIA WATOTO YATIMA KATIKA KITUO HIKI

Hiki ni kituo cha kulelea watoto Yatima kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam, ambacho kinamilikiwa na Mwanamama mpenda watoto na amani. Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2000 kikiwa na jumla ya watoto 17 huku lengo la Mwanamama huyo likiwa ni kutimiza hazma yake ya kulea watoto 150. Hadi sasa Kituo hicho kina jumla ya watoto 107 na kinalea watoto wa aina zote yaani Wavulana kwa Wasichana, Waislamu na Wakristo, Hivyo basi iwapo umeguswa na unahitaji kusaidia chochote ulichonacho kama ambvyo nimeguswa mimi hadi kufikia kupiga picha bango hili na kuandika na wala si wahusika waliohitaji kutangaziwa hivi, basi waweza kuwasiliana Mkurugenzi wa Kituo hicho, kwa Namba-0754 202216/0715 202216/0759 571079 ama barua pepe newlifeorphanshome2000@yahoo.com ama waweza kutembelea website yao www.newlifeorphanshome.com

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.