Habari za Punde

*SHEREHE ZA KUAPISHWA DK. SHEIN ZANZIBAR LEO

Rais wa awamu ya saba wa Serikali ya mseto wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akiapishwa wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo. katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya sita, Aman Abeid Karume.

Rais wa awamu ya Saba wa Serikali ya Mseto wa Zanzibar, Dk. Ali Mohame Shein, akikagua gwaride baada ya kuapishwa wakati wa sherehe za kuapishwa zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani leo.

Wanachama wa CCM na wa CUF, wakiwa waketi pamoja ndani ya uwanja wa Aman, wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar zilizofanyika mjini Zanzibar leo.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akiteta jambo na Salim Ahmed Salim, wakati wakiwa katika jukwaa kwenye sherehe hizo za kuapishwa kwa rais wa awamu ya saba ya Zanzibar, zlilozofanyika kwenye uwanja wa Amani.
Sehemu ya wananchi na wageni waliojitokeza kuhudhulia sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiongozana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, wakati wakiondoka kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya saba ya Zanzibar.
Rais waTanzania Dk. Jakaya Kikwete, akisalimiana na wananchi wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Amani katika sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar zilizofanyika leo.
Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, akiondoka kwenye Uwanja wa huo wa Amani mjini Zanzibar baada ya kumalizika kwa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya saba ya Serekari ya mseto.
wa awamu ya saba wa Serikali ya Mseto wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akiondoka na msafara wa magari na pikipiki akiongozwa na king’ora baada ya kuapishwa wakati akitoka kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Kijana akiwa amesimama na bango lake lililo na ujumbe kama linavyosomeka, akiwa nje ya uwanja wa Amani
Ni Sebene la Dufu tu kwenda mbele...

“MLISEMA MPEMBA HAONGOZI MSETO UMEKOLEA NAZI"

Hivi ndivyo walivyokuwa wakiimba wanachama hawa wa CUF wakati wakitoka uwanja wa Amani katika sherehe za kuapishwa Rais wa Zanzibar jana, huku wakiimba na kucheza Dufu wakielekea maeneo ya katikati ya mji wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.