Habari za Punde

*MISS EARTH, ROSE SHAYO AENDA VITNAM KUIWAKILISHA TANZANIA

Mwandishi wetu
MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth 2010, Rose Shayo aliondoka nchini kwenda Vietnam huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.
Akizungumza kabla ya kuondoka, Rose alisema kuwa amejiandaa viliyvyo chini ya muandaaji ake, Maria Sarungi wa Compass Communications and bila shaka atafanya vyema katika mashindano hayo.
Rose amesema kuwa haendi kuwa msindikizaji katika mashindano hayo na atafanya kila aliwezalo ili kufanya vyema kama ilivyokuwa kwa Miriam Odemba mwaka 2008 nchini Philippines.
“Najua kuna kushinda na kushindwa, mimi sitarajii kushindwa kutokana na maandalizi yangu, nawaomba Watanzania wanipe sapoti kubwa wakati wote nikiwa kambini na siku ya mashindano,” alisema Rose.
Maria alisema kuwa, alisema mrembo huyo amejiandaa vizuri kwakuwa mashindano ya kumsaka mrembo huyo yalifanyika mapema mwaka huu.
“Mashindano ya kumsaka mrembo huyu yalifanyika tangu mwezi wan nne mwaka huu kutokana na hali hiyo alipata muda mwingi wakujiaandaa hali inayomuweka katika nafasi nzuri ya kushinda, tutarajie ushindi kwakweli,” alisema Maria.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.