Habari za Punde

*APATA AJALI NA FAMILIA YAKE AKIENDA KATIKA IBADA YA KRISMAS LEO

Raia wakitoa msaada kwa mwanadada aliyeonyesha kuishiwa nguvu baada ya kupata ajali leo asubuhi wakati akiwa kwenye gari ndogo na familia yake wakielekea Kanisani.
Askari wa ulinzi, akitoa msaada wa huduma ya kwanza kwa mwanamke mjamzito, aliyepata ajali kwenye makutano ya Barabara ya Sokoine Drive na Ohio, wakati akiwa na familia yake wakielekea katika ibada ya Sikukuu ya Krismas leo asubuhi. Ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajiri T568 BFT na T213 BNR.
Gari lililokuwa likiendeshwa na mume wa dada huyo, baada ya kupata ajali hiyo.
Gari lililosababisha ajali hiyo baada ajali, ambapo magari yote yalipasuka rejeta.
Askari wa Usalama Barabarani, akiwasikiliza madereva wa magari hayo yaliyogongana asubuhi ya leo.
Madereva wa magari hayo kila mmoja akiwa bize kupiga simu kuwasiliana na ndugu na jamaa kutoa taarifa.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.