Wanafunzi hao walioandaa mgomo huo wa kutoingia madaraani kwa kile wanachoadai kukosa sehemu za kufanyia Fild, walianza kuandaa mgomo huo toka jana usiku mida ya saa tano kwa kuamshana madarasani na kupanga mikakati ya kufanya tukio hilo.
Tukio hilo la mgomo likiwa ni la kwanza kutokea chuoni hapo tangu kilipoanzishwa Chuo hicho, limezua tafrani baada ya wanafunzi hao kutawanywa kwa mabomu na wengine kukamatwa na polisi na kufikishwa vituo vya polisi vya mkoani humo, huku wengine wakitimkia maporini kusikojulikana.
Wakizungumza na Sufianimafoto kwa nyakati tofauti baadhi ya wanafunzi hao, waliotimkia maporini, ambao wengi wao wamejeruhiwa kwa kuchomwa na miba kutokana na kukimbia maeneo hayo bila viatu, wamedai kuwa hadi hivi sasa bado hali si shwari chuoni hapo na mabweni mengi yamebaki matupu.
“Sisi tunadai haki yetu kwani Chuo kimekuwa hakina utaratibu wa kueleweka kimekuwa kikiwaandalia Fild baadhi ya watu wanaochukua kozi fulani tu na wengine tumekuwa tukikosa kuandaliwa wala hatupewi hata barua za kutusaidia kupata sehemu za kufanyia fild”, alisema mmoja wa wanafunzi hao kwa njia ya simu.
No comments:
Post a Comment