Habari za Punde

*JK AMUAPISHA JAJI MKUU OTHMAN CHANDE LEO

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mohamed Othman Chande, kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake, Agustino Ramadhani.
'Kikao kisicho rasmi', Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dk Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anna Makinda, wakiteta jambo wakati wakiwa katika mkao wa faragha kwenye hafla hiyo.
Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, akikabidhiwa zawai ya maua na wanandugu, baada ya kuapishwa rasmi.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia hafla hiyo ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu, wakiwa kwenye Viwanja vya Ikulu, wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, (kushoto) akimpongeza jaji Mkuu baada ya kuapishwa (nyuma yao) ni Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisalimiana.
Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu, Othman Chande, wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu, baada ya zoezi la kuapisha.
Rais Jakaya na Jaji Mkuu, wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufaa.
Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu, wakiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Jaji Mkuu, baada ya kuapishwa.
Picha adimu ya Wakuu wa nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.