Habari za Punde

*KAMPUNI YA ALTAF YA JIJINI YAMPIGA TAFU SUPER D, KUHUDHULIA KOZI YA UKOCHA YA BFT

Mkurugenzi wa Kampuni ya Altaf & Company, Zulfiqal Ali akimkabidhi Pesa Taslim shilingi 150,000 Kocha wa mchezo wa Ngumi, Rajabu Mhamila (Super D) kwa ajili ya kwenda kushiriki mafunzo ya Ukocha yaliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT). Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam leo (katikati) ni Mke wa mfadhili huyo, Fatuma Zulfiqal.


Super D, awezeshwa kushiriki kozi ya ukocha ya BFT

Na Sufianimafoto Reporter, Dar

KOCHA wa Ngumi wa Klabu ya Ashanti ambaye pia anatoa mafunzo ya kujitegemea Rajabu Mhamila 'Super D' leo amekabidhiwa msaada wa Sh. 150,000 kwa ajili ya kumsadida kushiriki kozi ya siku 10 ya ukocha iliyoandaliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).

Msaada huo ambao ni wa pili kwa kocha huyo kupewa na kampuni hiyo, ulitolewa na mdau wa michezo Zulfiqal Ali, ili kumwezesha Super D kufanikisha malengo yake ya kuendeleza mchezo wa ngumi kwa vijana baada ya kushiriki kozi hiyo itakayoanza Desemba 14 hadi 24 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam na Sufianimafoto leo mchana, wakati akimkabidhi pesa hizo, Zulfiqal alisema ameamua kufanya hivyo ili kuungana na wadau wengine wa michezo pamoja na kuunga mkono kaulimbiu ya Serikali ya kuendeleza michezo nchini.

"Michezo ni ajira kwa vijana wetu na ili tuweze kufanikisha zaidi tunatakiwa kuwawezesha walimu kwanza ambao watatoa mwanga na mafunzo ya kina kwa wengine ndio maana nimeguswa katika hili na kusaidia.," alisema.

Hata hivyo Zulfiqal amewaomba wadau wengine kujitokeza kuungana na jamii kusaidia kukuza michezo ili kuwawezesha vijana wasio na ajira waweze kujiajili.

Naye Super D alisema anashukuru na kuahidi kuzingatia kozi hiyo siku zote ili aweze kupanua ujuzi ambao utawawezesha kuwasaidia mabondia wanaochipukia hapa nchini.

Awali kocha huyo alipewa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani zaidi ya shilingi laki tatu kwa ajili ya mazoezi ya mabondia wanaohudhuria mafunzo yanayotolewa na kocha huyo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.