Habari za Punde

*WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI, MATHAYO, AKAGUA MAZINGIRA YA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David (katikati) akiangalia na kushangaa magogo yanayotumika wakati wa kucharanga vichwa vya ng’ombe katika Machinjio ya Vingunguti Dar es Salaam. Waziri huyo leo alitembelea machinjio hayo na kujionea mazingira yaliyokithili kwa uchafu ndani ya machinjio hayo.
Ofisa Mifugo wa Manispaa ya Ilala, Dk. Assenga Sevenne (kulia) akimuonyesha Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David Mathayo, eneo linalotumika kushushia wanyama wanaoingia katika machinjio hayo kuchinjwa, wakati Waziri huyo alipotembelea Machinjio hayo leo mchana baada ya wachinjaji kugoma kuendelea na uchinjaji kwa siku kadhaa sasa kutokana na kile wanachodai Uongozi kutoboresha mazingira ya kufanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.