Nurdin Bakar, akishangilia bao lake la kwanza.Timu ya Kilimanjaro Stars, leo imewatoa kimasomaso watanzania kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Burundi katika Michuano ya Kombe la Tusker Challenge, inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kili imepata ushindi huo kwa kufunga mabao 2, yote yakifungwa na Nurdin Bakar kwa kichwa huku bao la kwanza akifunga kufuatia krosi ya Winga machachari Mrisho Ngasa na la pili akifunga pia kwa kichwa kufuatia krosi ya beki wa kulia Shadrack Nsajigwa katika dakika ya 75 ya mchezo.
Nurdin akionekana ni mwenye kismati ya magoli leo, katika dakika ya 69 alikosa goli la wazi baada ya kupewa pande na Mrisho Ngasa, huku yeye akiwa uso kwa uso na goli na kujaribu kumchambua golikipa lakini haikuwa bahati yake kwa kufunga kwa mguu bali ilikuwa ni bahati yake kufunga kwa kichwa tu katika mchezo wa leo kwa mpira huo ulitoka nje sentimita chache.
Kwa ushindi huo sasa Kilimanjaro imeingia hatua ya Robo fainali, ambapo inasubiri matokeo ya michezo ya kesho kati ya Ivory Coast, zanzibar na Sudan.

No comments:
Post a Comment