Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Aurola Security, Shomari Kimbau (katikati) akiwatambulisha mabondia, Sued Willson ‘Kiza Kinene’ (kushoto) na David Michael, wanaotarajia kupambana katika uzinduzi wa mchezo mpya wa Mapambano Mseto (Mix Fighting) utakaofanyika Desemba 31 kwenye Ukumbi wa DDC Mlimani Park Mwenge jijini Dar es Salaam. Utambulisho huo ulifanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Aidha Shmari alisema kuwa mpambano huo utakaokuwa wa raundi 5, ambapo utakuwa ni ufunguzi rasmi wa mchezo huo ambao kwa nchini bado haujatambulika sana kwa mashabiki wamichezo ya kupigana.
Katika mchezo huo pia kutakuwa na michezo ya utangulizi ya ngumi, baina ya Bondia Chipukizi, Thomas Mashallah na Said Mbelwa, wa uzito wa Midle Waight watakaochapana kwa raundi 10.
No comments:
Post a Comment