Habari za Punde

*MARIAM AIBUKA KIDEDEA BONGO STAR SEARCH ANYAKUA KITITA CHA SH. MILIONI 30

Mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Mariam Mohammed, akiwa na furaha iliyopitiliza baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo katika fainali zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. nyuma yake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Produaction, Rith Poulsen, akimpongeza kwa ushindi huo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 30, mshindi wa fainali za shindano la Bongo Star Search, Mariam Mohammed, baada ya kutangazwa mshindi. Katikati ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production, Ritha Poulsen.
Ofisa wa Mtandao wa simu za mkononi wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 10, mshindi wa pili wa fainali za shindano hilo, James Martine, ambapo pia Beatrice alikabidhi na zawadi ya mshindi wa tatu hundi ya Sh. milioni 5 na hivyo kufanya kampuni hiyo kutoa jumla ya Sh. milioni 15 katika fainali hizo.
Shabiki wa Mariam, aliyeshindwa kuvumilia na kuamua kupanda jukwani kumsaidia kusebeneka na miondoko ya Taarab.
Huyu wala si Miss tanzania akipita jukwaani na vazi la ufukweni la Hasha ila ni shabiki akitoka kumtunza msanii wake jukwaani katika fainali hizo baada ya kukunwa na miondoko.
Huyu pia ni Msanii wa Luninga, ambaye pia alivutiwa na mmoja wa wasanii na hasa Mariam, na kuamua kuinuka na kwenda kumtunza jukwaani.
Mshiriki James Martine, akiwapagawisha mashabiki wake na miondoko ya wimbo wa Kitambaa Cheupe wa King Kii ama kwa hakika walipagawa kweli na kibao hicho.
Eeeh! ndiyo si wote waliokuwa na kitambaa cheupe ila wengine walikuwa na viatu vyeupe na kuamua kuvua na kumsapoti James, ilimradi tu wameinua kitambaa cheupe kama huyu jamaa (kulia) akipeperusha raba yake nyeupe baada ya kukosa kitambaa.
Mariam, akiwapagawisha mashabiki wake jukwaani na miondoko ya Taarab.
Mshiriki aliyeshika nafasi ya nne katika shindano hilo, Bella, akiimba jukwaani.
Mshiriki aliyeshika nafasi ya tano katika fainali hizo, Waziri Salum, akishambulia jukwaa kwa nguvu zote.
Mzungu Kichaa akiimba kwa hisia wakati wa fainali hizo na kuwateka mashabiki wake ambao muda wote walikuwa hai kwa kumshangilia kila alipopanda jukwaani.
Eee, kama hivi mashabiki wengine wao walikuwa na mabango tu mwanzo mwisho kumtaka mzungu ashinde.
Miss Tanzania 2009, Nasreen Karim, akiwa na warembo wenzake ukumbini humo wakifuatilia fainali hizo.
Hapa ilikuwa ni ubishani na upinzani wa hali ya juu baina ya Majaji hawa, Ritha na Master J, hapa Ritha akimkalisha kwa nguvu Master J, baada ya kusimama na kumsifia msanii ampendaye na kuibua ubishani.
Hawa ni Warembo waliokuwa wakitoa huduma ukumbini humo, wakipozi kwa picha.
Huyu ni mmoja kati ya washiriki ambao hawakubahatika kuingia katika hatua ya tano Bora, akiimba kipande chake katika wimbo waliorekodi kwa pamoja wa ukimwi.
Mashabiki wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa jukwaani.
Mcheki huyu jamaa badala ya kuangalia jukwaani burudani iliyokuwa ikiendelea, yeye na Inye tuuuu.
Jaji Salama Jabri, akitoa pointi zake kwa mshiriki.
Si kwamba kwamba ananyanyua chuma la hasha ni staili ya kushangilia.





















No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.