Habari za Punde

*MPIGANAJI ABUU MKONGO WA ARUSHA, AFARIKI DUNIA

Na Mwandishi Wetu,Arusha.

MPIGA picha wa kituo cha Television cha ITV, mkoani Arusha, Abuu mkongo(34), juzi amefariki dunia baada ya gari alikuwa amepanda pamoja na ndugu zake watano kupinduka katika kijiji cha kileo wilayani Mwanga akitoka Arusha.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Lucas Ng'oboko alithitisha jana kutokea ajali hiyo saa tano usiku, baada ya gari walilokuwa wamepanda lenye namba za usajili T391PMQ aina ya Toyota Subaru kupasuka taili ya mbele na kuanguka.
Kamanda Ngoboko alisema gari hili lilikuwa linaendeshwa na kaka yake mpiga huyo,Baraka Mkongo(35) na kabla ya kupinduka lilikuwa likilipita gari jingine.
"katika ajali hii,watu wengine watatu walijeruhiwa akiwepo mtoto mdogo na bado wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi"alisema Ng'oboko.
Mpiga picha huyo, alikuwa akifanya kazi na mwandishi na mtangazaji wa ITV, Mwanaidi Mkwizu ambaye alisema kabla ya ajali hiyo, Mkongo alimuaga kuwa anakwenda nyumbani kwao Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya dua ya wanafamilia.
Kamanda na polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye jana aliungana na wanahabari wa Arusha katika msiba huo na kutoa pole ya sh,100,000 ambapo pia aliwatakia safari njema wanahabariambao leo watakwenda Mwanga kwenye maziko.
Katika salamu zake za rambirambi Kamanda Andengenye aliwataka waandishi wa habari mkoani Arusha kuendelea kuonyesha zaidi katika kipindi hicho cha mziba.
Katika hatua nyingine Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) kimetoa pole kwa waandishgi wa habari,ndugu, jamaa na wanafamilia ya marehemu Mkongo.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.