Habari za Punde

*TASWA FC YAWAADHIBU WAANDISHI WA NJE 8-1

Kikosi cha Timu ya Taswa Fc, kilichowasambaratishwa waandishi mchanganyiko wa nje katika mchezo wa kirafiki kwa mabao 8-1, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam. Kutoka (kushoto) waliosimama ni Julius Kihampa wa gazeti la Majira na Dar Leo, Shafii Dauda wa Clouds Tv na Radio, Salum Jaba- Mwananchi, Saleh Ally- Global Publishers, Majuto Omar- The Citizen, Ally Mkonge- ITV na Redio One. Mbele kutoka (kushoto) ni Mduma, Kulikoni, Sweetbart Lukonge- Mwananchi, Willbroad Moland- Champion, Muhidin Sufiani-Bingwa na Mtanzania, na Sultan Sikilo, Redio Times.
Kikosi cha Waandishi wa nje.
Sufianimafoto (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na washkaji kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Sufianimafoto, ambaye ni beki wa kulia wa Taswa Fc, (kushoto) akimiliki mpira huku mshambuliaji wa timu ya waandihi mchanganyiko wa nje, akijiandaa kumkabili.
Sufianimafoto, akimfinya mtu.
Kiungo mshambuliaji wa Taswa Fc, Saleh Ally, akijiandaa kukanyaga shuti la maana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.