Habari za Punde

*TID ALIVYOFUNIKA KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YAKE YA SIFAI

Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 4 lililofanyika mwaka 2009, Kevin Chuwang Pam, kutoka nchini Nigeria (katikati) akiimba na kucheza na msanii wa muziki wa kizazi kipya, TID, wakati wa uzinduzi wa albam ya nne ya msanii huyo, inayokwenda kwa jina la Sifai. Kulia ni Elizabeth Gupta, ambaye ni mchumba wa Kevin, wachumba hao walialikwa jukwaani na kutangaza kuhusu uchumba wao, ambapo wanataraji kufunga ndoa hivi karibuni. Uzinduzi huo ulifanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Club Billicanas Dar es Salaam.
TID (kulia) akishambulia jukwaa na AY, Mzee wa Comercial...
Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID, akionyesha umahiri wake wa kucheza ‘Breack Dace’ jukwaani, wakati wa onyesho la uzinduzi wa albam yake ya nne mpya inayokwenda kwa jina la Sifai, iliyozinduliwa kwenywe Ukumbi wa Club Billicanas.
Wasanii wa Kikundi cha Bombeso, wakionyesha umahiri wao jukwaani wakati wa uzinduzi huo.
Shabiki akimtunza Lady Jay Dee, wakati alipopanda jukwaani ikiwa ni sehemu ya kusindikiza mama kusherehesha uzinduzi huo.
Huyu naye, alikuwapo...wanamuita Bilali Mashauzi ama Aunt Bilal, hapa akijishebedua na kutoa hela kumtunza shost wake...

HUYU DADA NAYE ALIWAPAGAWISHA WATU KINOMAAAA!
Shabiki wa muziki wa Taaraba, Mwanadada akicheza mduara na mwanamuziki wa Top Band ,wakati wa uzinduzi huo, ama kwa hakika Mdada huyu alikuwa kivutio kwa kila shabiki wa muziki aliyeingia ukumbini humo kwa jinsi alivyokuwa akizungusha vilivyo nyonga kwa kufuata midundo ya muziki huo.
Eeeeh! si unaona??? Hadi Madada wenzake walipagawa naye na kuamua kwenda kumtunza mahela..
Elizabeth akimpoza mumewe mtarajiwa Kevin, baada ya kushuka jukwaani.
Msanii wa kundi la Bombeso, akifanya vitu vyake katikati.
Mangwair, akiwa na mchuchu wake Mzungu, baada ya kushuka jukwaani kutoa sapoti katika uzinduzi huo.
Mashabiki wakiwa makini kucheki kila kinachoendelea jukwaani.
TID, akipozi katika picha na mashabiki wake wa ukweli...."Ahsanteni kwa kuja"
Baadhi ya mashabiki wakiwa ukumbini humo.
Mwimbaji wa Top Band, Kidawa Abdul, akishambulia jukwaa.
Mashabiki wakijiachia ukumbini humo.
Hawa ni wale waliokuwa wakitaka kuona kwa ukaribu zaidi na kuamua kuketi eneo la kuchezea muziki ili kuweza kuona kwa ukaribu zaidi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.