Habari za Punde

*AFA KWA KUPIGWA RISASI YA KICHWA, MAJERUHI KWA RISASI YA KIUNO

RPC wa Mkoa wa Mbeya Advocete Nyombi na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani James Kombe (kulia)


Na Francis Godwin, Iringa

Mtu mmoja mkazi wa Ubaruku Wilaya ya Mbarali, aliyetambulika kwa jina moja la Justine, amekufa papo hapo baada ya kupigwa risasi ya kichwa na mwingine kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi ya kiuno wakati wa vurugu kati ya wananchi wa Kijiji cha Ubaruku na Polisi .
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Kamanda Mkuu wa Wialaya ya Mbarali Kanali Cosmas Kayombo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Advocate Nyombi zilisema kuwa tukio hilo limetokea leo mchana baada ya wananchi wa eneo hilo kuzuia lori la tani 10 kuingi katika eneo hilo kama serikali ya wilaya ilivyopata kupiga marufuku malori hayo kuingia maeneo yao.
Aliyejeruhiwa kwa risasi katika tukio hilo ametambuliwa kwa jina la Husein na kuelezwa kuwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mbarali kwa matibabu.


Pia wananchi hao wameteketeza kituo cha mafuta kinachomilikiwa na mfanyabiashara mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Mnishi pamoja na kuchoma moto lori moja kati ya hayo yaliyozuiliwa.
Hata hivyo inadaiwa kuwa wananchi hao walifikia hatua hiyo ya kuzuia lori hilo ambalo ni mali ya watu wenye rangi nyeupe kutokana na kuwepo kwa upendeleo ambapo wananchi wenye ngozi nyeusi wamekuwa wakipigwa marufuku malori yao kuingia eneo hilo kwa usalama wa barabara huku wengine wenye pesa wakiruhusiwa kuingiza malori yao.
Wakati wananchi wakidai kuwa polisi ndio ambao wamehusika na mauwaji hayo na kujeruhi wananchi hao kwa risasi ,jeshi la polisi bado halijasema lolote juu ya tukio hilo na kudai kuwa bado linafanya uchunguzi zaidi.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.