Habari za Punde

*CHADEMA IRINGA WAMPIGA STOP MGOMBEA UDIWANI WA KATA YA KWAKILOSA

Na Francis Godwin, Iringa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini kimetangaza kumsimamisha uanachama na kumfukuza ndani ya chama hicho aliyekuwa mgombea udiwani wa Kata ya Kwakilosa jimbo la Iringa mchini Abumeleck Changawa, kutokana na utovu wa nidhamu dhidi ya mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa.Changawa anadaiwa pamoja na kukikosea heshima chama hicho na wananchi wa jimbo la Iringa mjini ambao walimchagua mchungaji Msigwa kama mbunge wao bado alimdhalilisha mbunge huyo kwa kumtoa katika gari yake na kumtupa nje ya gari walilokuwa wakisafiria pamoja na mbunge huyo.Akitoa tamko la chama mbele ya waandishi wa habari leo ofisini kwake katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonokulima (pichani kulia)alisema kuwa chama kimelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kutoafiki tabia ya mwanachama huyo mwenye kadi namba 0234984 ambaye kwa makusudi amekuwa akiendelea kukichafua chama na mbunge Msigwa.Katibu huyo alisema kuwa Changawa ameendelea kutoa lugha chafu dhidi ya mbunge huyo ikiwa ni pamoja na kutoa vitisho jambo ambalo baraza la wazee wa chadema ,na kamati ya utendaji ya chama kuamua kukutana na kutoa tamko dhidi ya mwanachama huyo.Hata hivyo alisema kuwa Changawa katika taarifa zake za kumchafua mbunge Msigwa ambaye pia ni mwenyekiti wa wilaya wa Chadema alimtaka mchungaji Msigwa kama mwenyekiti wa Chadema wilaya kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai kuwa ni msimamo wa waliokuwa wagombea udiwani wa Chadema jimbo hilo jambo ambalo ni uzushi wake binafsi na sio msimamo wa wenzake.Katibu huyo alisema kuwa tayari kamati ya utendaji ,madiwani kivuli wamepata kukutana na kutoa mapendekezo yao yanayokiagiza chama kuchukua hatua ya kinidhamu ya kumwajibisha mwanachama huyo.Akitoa uamuzi wa chama hicho wilaya katibu huyo Mgonokulima alisema kuwa kuanzia leo chama kimemsimamisha uanachama ndani ya chadema mwanachama huyo Changawa .Mgonokulima alisema kuwa katika kikao kilichoketi Januari 16 mwaka huu baada ya chama kujiridhisha na mtiririko wa makosa ya makusudi ya utovu wa nidhamu kwa chama chenyewe na kwa kiongozi huyo wa chama na mbunge wa jimbo la Iringa mjini ,kimelazimika kumsimamisha uanachama Changawa kwa kusema ovyo dhidi ya chama kinyume na katiba ya chama hicho.Hata hivyo chama kimetoa muda wa siku 7-14 kwa Changawa kujibu kwa maandishi sababu za kukosa nidhamu na iwapo atashindwa kufanya hivyo atakuwa amejivua uanachama ndani ya chama hicho na chama kitampokonya kadi ya uanachama .Kwa upande wake Changawa alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea barua yoyote toka chama inayomtaka kujieleza na kuthibitisha kuzungumza na vyombo vya habari juu ya mawazo yake ya kumtaka mbunge huyo kuachia nafasi ya ue nyekiti ili kubaki na nafasi moja ya ubunge kama sehemu ya kuachia majukumu kwa wengine wenye sifa.Kuhusu kutakiwa kurejesha kadi ya chama hicho iwapo siku 14 zitapita bila kujieleza juu ya suala hilo ,Changawa alisema kuwa hadi sasa yeye hana kadi ya Chadema na kuwa kadi ipo kwa mbunge huyo na kuwa hata fomu yake ya kugombea udiwani ilijazwa na mbunge Msigwa na kuwa namba ya kadi yake haitambui na kuwa yupo tayari kuondoka ndani ya chama kama viongozi wataendelea kutetea uovu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.