Na Mwandishi Wetu, Kiteto
NYOKA aina ya Chatu kwa zaidi ya miezi mitatu ,anatishia maisha ya wakazi wa Kitongoji cha Kazaroho,Kijiji cha Matui,Wilayani Kiteto,Mkoani Manyara na kuwasababisha kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo na wengine kujifungia ndani ya nyumba zao kwa kuogopa kukutana na nyoka huyo
Wakazi hoa wameiomba Serikali kupitia idara ya wanyamapori kumsaka nyoka huyo na kumuondoa katika makazi yao ,hivyo kuwawezesha kuendelea na miradi ya maendeleo na biashara zao bila hofu .
Wakizungumza na waandishi wa habari,wakazi hao walidai kuwa nyoka huyo anayekadiriwa kuwa na uzito wa kilo 80, amekuwa akifanyiwa tambiko na wenyeji wa kabila la warangi na wagogo kwa kumpa unga na maziwa ili asilete madhara ndani ya kijiji hicho.Mmoja kati ya wakazi hao alisema kuwa nyoka huyo ana zaidi ya miezi mitatu hapo kijijini na wazee maarufu walipomwona waliwataka wananchi wasimdhuru kwani kuna masuala ya kimila ambayo walitaka kufanya."Kwa kipindi chote hicho makabila ya warangi na wagogo wamekuwa wakishughulika naye lakini baada ya kuanza shughuli za kilimo watu wamepata hofu kubwa kuwa huenda akaleta madhara kwa jamii," alisema.Akithibitisha kuwepo kwa nyoka huyo ambaye wananchi wanahofu hata kwenda kufanya kazi za kujiletea maendeleo diwani wa kata hiyo Kidawa Othmani (Obama) alisema amewasiliana na maafisa wa mali asili ili wamuondoe nyoka huyo.Othmani alisema kutokana na malalamiko ya wananchi kuwa hawawezi kuamini usalama wao wamemitaka kutoa taarifa ili nyoka huyo aondolewe hapo kijijini na siyo kuuawa ili waweze kufanya shughuli zao kwa amani."Kwa kweli hali sio shwari hasa kipindi hiki cha kilimo ambapo kila mtua anataka kwenda kufanya kazi zake huko maporini, sasa wanapokutana na nyoka huyo mara kwa mara inawatisha"alisema Diwani huyo maarufu (Obama).Alisema alipowasiliana na maafisa hao hadi jana walikuwa hawajafika na kwamba ameitaka serikali inapojulishwa juu ya hatari ndani ya jamii ifanye haraka kabla ya kujitokeza madhara."Nimeongea nao mwenyewe asubuhi (maafisa wa mali asili) wakasema wanakuja lakini hadi sasa (jana) jioni walikuwa hawajafika hali hii inaweza kubadilisha matokeo kwa aidha kutokea madhara"alisema Diwani huyo.Kwa upande wa maafisa hao wa maliasili wa wilaya wakizungumza na waandishi wa habari kwa masharti ya kutotajwa majina walisema wanampango wa kwenda huko kuona nyoka huyo ili waweze kumwondoa kijijini hapo.

No comments:
Post a Comment