Habari za Punde

*KILIMANJARO PREMIUM NA BASATA WAZINDUA RASMI TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mchana, wakati wa uzinduzi rasmi wa Tuzo za Wasanii waliofanya vizuri kupitia kazi zao, yanayotarajia kufanyika Machi 26 mwaka huu ‘Kilimanjaro Music Awards’. Kushoto ni Mratibu wa Tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa BASATA, (kulia) ni Mratibu Msaidizi wa maandalizi ya Kilimanjaro Music Awards, Edith Bebwa.

KILIMANJARO PREMIUM LAGER na BASATA leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2010.

Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo yataendelezwa na kuboreshwa zaidi mwaka huu. Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua zifuatazo:

1. ACADEMY:

ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki mia moja (100) kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa vinyang’anyiro (categories) mbali mbali. Utaratibu huu haujabadilika na mwaka huu utafanyika tarehe 12 na 13 Februari 2011.

2. Majaji:

Majaji hua na kazi moja kubwa ya kuhakiki uteuzi wa Nominees uliofanyiwa na Academy ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2010, kazi zao za mwaka 2010, Mafanikio n.k n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa muziki 15.

3. KURA:

Kura za wapenzi wa Muziki nazo hujuishwa katika kuchangua washindi. Mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia 50 na majaji asilimia 50. Njia za kupiga kura ni pamoja na:

- SMS.

- Email.

- Magazeti.

- Fliers.

Wawezeshaji:

Kilimanjaro Premium inaendelea kufanya kazi na makampuni matatu katika mchakato na uwezeshaji wa Tunzo za Muziki. Makampuni haya ni pamoja na:

1. Digital Arts – Wasimamizi wakuu wa mchakato wa Tunzo.

2. 1Plus Communications – Wasimamizi wa mawasiliano ya wasanii pamoja na umma.

3. Entertainment Masters – Wasimamizi wa burudani na mahitaji yake.

4. Deloitte Management Consulting – Wasimamizi na wahakiki wa mchakato wa upatikanaji wa wateule pamoja na washindi wa Tunzo za Muziki Tanzania.

Mchakato wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2010 kwa tarehe:

Maelezo ya ziada:

Mwaka huu Kilimanjaro kama mdhamini imeamua kuwarudishia wadau na wapenzi wa muziki wa Tanzania usiku wa tunzo. Burudani yote ya usiku huo itatolewa na wasanii wa hapa nyumbani tu. Hapatakuwa na msanii kutoka nje ya nchi kwa vile wasanii wetu wa ndani wanaweza na wanatosha ukizingatia ni Tunzo zao.

Kwa maelezo zaidi

1Plus Communication, P.O Box 978, Simu: +255 222 780 016 Mikocheni B, Dar es Salaam, Tanzania, email: info@oneplus.co.tz.

George Kavishe, Brand Manager, +255 767 266786, George.kavishe@tz.sabmiller.com

Kuhusu TBL

Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Pilsner Lager na Tusker Lager. Bia nyingine kubwa zinazotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Konyagi Ice.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vitatu vya bia, kiwanda kimoja cha vinywaji vikali, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller

SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabar matano. Bia zake ni pamoja na zila za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.

SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya nchini Uingereza na Johannesburg.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.