Habari za Punde

*KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KUTINGA MAHAKAMANI KUZUIA KULIPWA KWA MABILIONI YA FEDHA KWA KAMPUNI YA DOWANS

Mkurugenzi wa wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Francis Kiwanga, akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, kuhusu uamuzi wa kwenda mahakama kuu kuzuia serikali kuilipa Kampuni ya Dowans mabilioni ya fedha kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Biashara. Kushoto ni Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya. Picha kwa Hisani ya Chachandu Daily

KITUO cha Sheria na Haki za Bianadamu (LHRC) kimeungana na baadhi ya wanaharakati kwenda Mahakama Kuu ya Tanzania leo, kuzuia amri ya Mahakama Biashara ya Kimataifa ya kutaka Tanesco ilipe Dowans Sh. bilioni 97.

Maamuzi hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kituo hicho, Francis Kiwanga katika mkutano na waandishi wa habari, katika Ofisi za kituo hicho, Kijitonyana jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.