Habari za Punde

*MANISPAA YA IRINGA YAKOSA LITA 10 ZA MAFUTA YA GARI LA TAKA

Na Francis Godwin, Iringa
UONGOZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoa wa Iringa, umesema kuwa umeshindwa kusomba takataka zilizorundikana mitaani kwa zaidi ya miezi miwili sasa kutokana na kukosa fedha za kununulia mafuta lita 10, kwa kila tripu moja ya gari hilo kuzunguka mitaani kuondoa taka hizo.
Kutokana na uongozi wa Manispaa ya Iringa kushindwa kuzoa takataka hizo katika vituo vya taka baadhi ya maeneo yakiwamo ya Isoka , Mtaa wa kwa Mwagongo na maeneo mbali mbali ya mji wa huo kwa sasa yamezungukwa na uchafu mwingi pamoja na harufu mbaya inayokera iliyosababishwa na takataka hizo jambo lililopelekea wananchi kutishia kuandamana hadi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa kulalamikia hali hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa maeneo hayo, walisema kuwa takataka hizo zimekuwa kero kubwa na kwamba zinatishia magonjwa ya mlipuko kutokana na harufu mbaya inayotokana na taka hizo na makaburi yaliyopo eneo hilo kufukiwa na taka hizo kutokana na uwingi wake.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Teresia Mahongo, Ofisa afya wa Manispaa ya Iringa Deodata Rukupwa, walisema kuwa kuwa ili gari hilo la kusomba takataka katika Manispaa ya Iringa liweze kuzunguka mitaani kusomba taka linahitaji kujaza mafuta lita 10 kwa kila mzunguko mmoja kutoka eneo husika kwenda kumwaga eneo la Kihesa kilolo nje kigodo na mji wa Iringa.
Hata hivyo mkurungenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa alipofuatwa na mwandishi wa habari hizi ili kuthibitisha madai hayo ya Manispaa ya Iringa kukosa fedha za kununulia mafuta lita 10 kwa ajili ya gari hilo aligoma kuzungumza na kumuwakia mwandishi wa habari hizi.
Taka hizo zikiwa zimetapakaa katika maeneo ya mji huo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.