Habari za Punde

*MATUKIO YA MKESHA WA KITAIFA WA MWAKA MPYA

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipanda jukwaani baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Mkesha wa Kitaifa, uliofanyika maalum kuukaribisha Mwaka mpya 2011 na kuuaga 2010.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya Viongozi wa Dini, wakipeperusha Bendera ya Taifa ikiwa ni ishara ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2011 na kuuaga Mwaka 2010, mara tu ilipotimu saa sita kamili usiku.
Brass Band ya Polisi wakiwatoa burudani ya muziki wa ala wakati wa Mkesha huo.
Mwandishi wa Redio ya Dini, akiwa na hisia na kutokwa na machozi wakati wa kuukaribisha mwaka mpya.
Watoto wa Kikundi cha Kanisa wakiandamana na maboksi yaliyokuwa yameandikwa ujumbe mbalimbali kuhusu maovu ambayo walikuwa wakiashilia kuyaacha muda mfupi kabla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2011, wakati wa Mkesha wa Kitaifa uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Watoto wa kikundi cha Kanisa wakicheza muziki wa Kwaya uwanjani hapo wakati wa mkesha huo wa Kitaifa.
Mtangazaji wa TBC Televisheni Msami, (mwenye suti nyeusi) akishambulia jukwaa kwa kucheza miondoko ya kwaya jukwaani wakati wa Tamasha la Mkesha wa Kitaifa uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ibada inaendelea huku baadhi ya watoto waliohudhulia mkesha huo wakiuchapa usingizi uwanjani hapo.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakiwa katika mkusanyiko wa Ibada ya Mkesha wa Kitaifa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal. Mkesha huo ulikuwa ni maalum kwa kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2011.
Wananchi wakiendelea kufurahia kuukaribisha mwaka Mpya.
Pia Wazee walikuwapo uwanjani hapo katika Ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya.











No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.