makadirio ya bajeti ya mji huo kwa mwaka 2011-2012 wakati wa kikaocha makadilio ya bajeti kilichofanyika jana.Picha fortunatha Ringo.
MAMLAKA ya mji mdogo wa Mirerani,wilaya ya Simanjiro,mkoani Manyara imewasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa kata mbili zinazounda mamlaka hiyo. Katika mapendekezo hayo bajeti ya maendeleo ya mwaka 2011-2012 ya mji mdogo wa Mirerani iliyokadiriwa kutumia kiasi cha sh2 Bilioni ilipitishwa na wajumbe wake. Ofisa mipango wa mji huo,Raphael Mawi,akisoma makadirio yabajeti hiyo hivi karibuni,kwa niaba ya Ofisa Mtendaji wa mji huo,AlbertNgala alisisitiza kuwa mgawanyiko wake umejikita kwenye miradi ya maji,elimu,barabara na mengineyo. Mawi alieleza kuwa kwenye ujenzi wamepanga kutumia sh 1.36Bilionikatika kutengeneza barabara za mitaa ya mji ambazoziliharibika kutokana na mvua za el nino na fedha hizowaliahidiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa. Alibainisha kuwa kwenye kilimo na mifugo wamepanga kutumia sh 86 milioni za uendeshaji mfereji wa shango,josho la mifugo,mbouti,banda la machinjio ya mbuzi,kuingiza umeme na maji machinjioni na nyumba ya mtumishi. "Tutatumia sh80 milioni kwenye mradi wa maji katika mitaa ya Songambele B na Sokoni,Songambele A na Mirerani pamoja na ujenzi wa tanki la maji," alifafanua Mawi. Kwenye elimu aliongeza kuwa watatumia sh 41 milioni kujenga madarasa matatu ya shule ya msingi Zaire na kujenga nyumba ya walimu wa shule ya sekondari Mirerani Mkapa.
No comments:
Post a Comment