Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi ,akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya maofisa wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Nchini baada ya kuitembelea Tume hiyo ijini Dar es Salaam leo. Pamoja na mambo mengine amesema kuwa tume hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kuthibiti uingizwaji wa biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na udhaifu wa sheria iliyopo ya kupambana na kuthibiti dawa hizo ambapo amesema kuwa Serikali imeanza mkakati wa kuunda timu itakayotoa mapendekezo kuhusu uimarishaji wa sera, muundo na urekebishaji wa sheria ya kudhibiti dawa za kulevya ya mwaka 1995, ili kutoa uwezo kwa Tume hiyo kuwashughulikia moja kwa moja wanaojihusisha na biashara hiyo. Picha Zote na Aron Msigwa- MAELEZO
Wizara ya Nishati, Equinor wakutana Afrika Kusini
-
Wizara ya Nishati Tanzania imekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya
Equinor Tanzania AS kujadili, pamoja na mambo mengine, maendeleo ya
utekelezaji wa...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment