Habari za Punde

*SHEREHE ZA MKESHA WA SIKUKUU YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Mwendesha Pikipiki akionyesha umahiri wake wa kucheza na pikipiki katika barabara ya Mlandege jana usiku ambapo kila mmoja aliweza kutembea kwa kutumia tairi moja hewani kwa umbali wa mita 500, ama kwa hakika ilikuwa ni burudani ya pekee kwa usiku huo. Sheree hizo limeazimishwa rasmi leo asubuhi katika Uwanja wa Amani na kuhudhuliwa na Viongozi wa Kiserikali.
Mwimbaji wa kundi la Taarab la Zanziba Big Star, Bahati Amad, akiimba wakati wa sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Mapinduzi zilizoandaliwa kwa ushirikiano wa Vyama vya Siasa vya CCM na CUF, zilizofanyika katika Viwanja vya Kisonge mjini Zanzibar jana usiku. Wazanzibari husherehekea mkesha huu wa sikukuu ya Mapinduzi ikiwa ni sawa na kuukaribisha mwaka mpya kama ambavyo hufanywa na watu wengine duniani siku ya tarehe 31 Desemba, wao siku ya tarehe hiyo ni ya kawaida mjini hapa na kusubiri mkesha wa tarehe 12 Januari ambapo hufanya yale yote yanayofanywa wakati wa kuukaribisha mwaka mpya ikiwa ni pamoja na kufyatua Baruti hewani pamoja na kusikika milio ya mizinga, michezo ya Pikipiki na Magari huku askari wakiwa wametanda kona zote za mji kuzuia vurugu nay ale yote yasiyoruhusiwa na katika Viwanja vya Kisonge hukusanyika watu kibao pamoja navikundi mbalimbali vya burudani huku kila kimoja kikipagawisha kwa stairi yake.

Wasanii wa Kikundi cha Zanzibar Stars, wakiimba katika Sherehe hizo jana usiku.

Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Kariakoo, kikiwapagawisha wakazi wa Zanzibar kwa ngoma yao ya Bomu kutoka Pemba, wakati wa sherehe hizo.
Baadhi ya wakazi wa mjini Zanzibar wakiwa katika mjumuiko wa watu waliohudhulia sherehe hizo kwenye Viwanja wa Kisonge jana usiku.
Mchezo wa Pikipiki Ukiendelea katika Barabara ya Mlandege...
Mashabiki wa mchuo wakishuhudia umahiri wa waendesha Pikipiki hao.
Askari wa kutuliza ghasia nao walikuwapo katika Mitaa ya mjini Zanzibar jana usiku kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia.
Baadhi ya wakazi wa mjini Zanzibar, wakiwa katika maeoneo ya Kisonge ambapo ni mahala maalum kwa Sherehe hizo zinazofanyika kila mwaka mjini Zanzibar.










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.