Tangazo lililochorwa kwenye ukuta wa Soko Kuu la Kariakoo, likiwa limefutwa kwa mtindo wa kuchafuliwa ili lisisomeke, na hii imeelezwa ni kutokana na anayehusika na tangazo hilo kushindwa kulipia gharama za kuendelea kutangaza katika nafasi hiyo na mahala hapo. Baada ya kufanya hatua hii inatakiwa mmiliki wa tangazo kufika na kufuta mwenyewe kwa muda aliopewa kabla ya kampuni husika kurejea tena na kuchukua hatua nyingine ambayo itakuwa ni gharama kubwa zaidi. Lakini mpaka kufikia hatua hii ya kuchafua mazingira inamaana wahusika yaani walipaji na walipwaji walikuwa hawafahamu mwanzo na mwisho wa mkataba na kuanza kukumbushana? au ndiyo dharau?
Ni uchafu tu mahala hapo.
Ni uchafu tu mahala hapo.
No comments:
Post a Comment