Watoto wa mitaani wakiwa wameuchapa usingizi katika Baraza la Jengo la Benjamini Mkapa, lililopo Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo mchana. Ongezeko la watoto wa Mtaani limekuwa likikuwa siku hadi siku, pamoja na kuongezeka kwa vituo vya kulelea watoto yatima lakini bado utazani ndoyo kwanza vituo hivyo vimefungwa. sasa basi ni nani wa kulaumiwa na nani mwenye jukumu la kuwaangalia watoto kama hawa? Ni Serikali ama Wazazi? Kwani si wote wanaozagaa mitaani kuwa ni watoto Yatima la hasha, wengine wamekimbia tu katika nyumba zao ama kwa mateso ya wazazi ama mmoja kati ya wazazi, ama ugomvi wa kila siku baina ya wazazi, ama njaa kali inayosababishwa na wazazi ama mmoja kati ya wazazi na maisha magumu kwa ujumla. Hadi hii leo ukiwa maeneo ya katikati ya jiji la Lukuvi kwa kweli huwezi kutembea hata hatua kumi kabla ya kukutana na angalau mtoto mmoja ambaye bila woga atakuface ili umsaidie chochote na kama huna basi hata mia na msemo wao ni "Naomba miambili nikale" na wewe hata kama si mzazi lakini lazima utajisikia huruma na kujisikia kumsaidia mtoto huyo, lakini je utawasaidia wangapi kwa siku hiyo kwani hutaweza kupiga tena hatua kumi kalba ya kukutana na mwingine na wewe ukizingatia umeondoka home na vijinauli vyako ulivyojipigia hesabu kuwa vitakusongesha hadi utakaporejea home jioni. NANI WA KULAUMIWA, SERIKALI kutowachukulia hatua kali Wazazi wanaosababisha mambo haya? ama WAZAZI WALIO HAI WANAOSASABISHA ONGEZEKO HILI?
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 28, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 28,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetin...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment