Habari za Punde

*WANANCHI WA MKOANI MBEYA WATEKETEZA BASI KWA MOTO

IGP MWEMA
Na Francis Godwin, Iringa
Wananchi wanao daiwa kuwa na hasira kali wakazi wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wameteketeza basi kwa moto baada ya basi hilo kumgonga mtembea kwa miguu.
Akizungumza kwa njia ya Simu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advotece Nyombi, alisema kuwa pamoja na wananchi hao kuchoma moto basi hilo bado wameweza kufunga barabara na kupelekea msongamano mkubwa wa magari katika eneo hilo la tukio.
Alisema kuwa tukio hilo limetokea leo na kuwa hadi sasa jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kuwasihi wananchi hao kutuliza jazba ili kufungua barabara hiyo.
Kamanda huyo alisema mbali ya mtu mmoja huyo aliyegongwa na basi hakuna mtu mwingine ambaye amepata kufa wala kujeruhiwa katika tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.