Habari za Punde

*WANANDUGU WAMUUA MFUGAJI WA KIMASAI KWA KIPIGO

Bibi wa kimasai akiwa katika mavazi maalum

Na Francis Godwin, Iringa
NGUDU wakazi wa kijiji cha Makifu wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua kwa kipigo mfugaji jamii ya kimasai marehemu Takasiko Mang'unaa .
Imeelezwa kuwa chanzo cha mauwaji hayo ni marehemu huyo kulazimisha kulisha mifugo yake ndani ya shamba la mazao la wanafamilia hao waliofanya mauwaji hayo.
Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kabla ya mauwaji hayo moja kati ya malalamiko makubwa ya wanadungu hao Majambo Mkala (77) na Yusitini Mkala (25) na juu ya mfugaji huyo kuchungia mifugoi yake ndani ya shamba lao.
Hata hivyo shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa wauwaji hao walitumia kitu chenye ncha kali mfano wa dispisi kumchoma kichwani marehemu huyo hadi alipopoteza maisha yake.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evalist Mangalla ametihibitisha kutokea kwa mauwaji hayo na kuwa tukio hilo lilitokea January 8 majira ya saa 11.45 jioni .
Pamoja na mashuhuda hao kudai kuwa wauwaji hao walitumia kitu chenye ncha kali katika kutekeleza unyama huo bado jeshi la polisi mkoa wa Iringa limedai kuwa marehemu huyo aliuwawa kwa kuchapwa fimbo katika sehemu mbali mbali za mwili wake.
Hata hivyo alisema wahusika wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika .


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.