Habari za Punde

*WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA SIKU 3 WA NSSF ARUSHA FEBRUARI 2

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, NSSF, Ludovick Mrosso, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa siku mbili wa wadau wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika mkoani Arusha kuanzia Februari 2 hadi 4, mwaka huu, ukiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili mfuko huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Said Masimango.

Na Naomi Mwainyekul, Jijini

WAZIRI Mkuu wa Tanzani, Mizengo Pinda, anatarajia kufungua mkutano wa siku tatu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la Taifa (NSSF) unaotarajia kufanyika jijini Arusha kuanzia februari 2 hadi 4 mwaka huu.

Maandalizi ya mkutano huo tayari yamekamilika na hivi sasa Shirika hilo liko katika hatua za mwisho za maandalizi ya mkutano huo kwa ajili ya kukutana na wadau wake.

Mkutano huo ambao ni wa kwanza wa aina yake, unaotarajia kufanyika katika ukumbi wa Internation Comference Centre (AICC) jijini Arusha.

Akizungumza na waandsihi wa habri jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mkutano huo unalengo la kujadili mada na changamoto mbalimbali za wadau wake ili kuzidi kuweka mausiano mazuli katika kuwaleta wadau wa NSSF kuwa karibu zaidi na kuboresha Shirika hilo.

Aidha alisema kuwa mkutano huo utawashirikisha wadau mbalimbali kutoka nchi tofauti za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Malaysia na Oman, ambapo jumla ya wageni pamoja na wenyeji wa mkutano huo utakuwa na jumla ya washiriki 600.

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajia kuwa waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.

Wajumbe wengine watakaoshiriki mkutano huo watakuwa ni waajiliwa, wakuu wa vitengo vya utawala na fedha wa maofisi mbalimbali na wataalam mbalimbali wa masuala ya jamii.

Mkutano huo wa siku tatu utakuwa ni kujadili hoja kadhaa Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, Mamlaka ya usimamizi wa mashirika ya jamii.

Shirika hilo litahakikisha washilika wa mkutano huo wanapewa nafasi ya kujadili kwa kina dukuduku zao kuhusiana na masuala ya NSSF.

Pia wataelimishwa kwa undani kuhusu sheria Na.28 ya mwaka 1997.

Aliwataka wadau wengi kujitokeza ushiriki katika mkutano huo ili kujadili na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazolikabiri Shirika hilo.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.