Askari wa Usalama Barabarani, (kulia) wakiangalia ajali iliyohusisha magari matatu ya Scania lenye namba za usajiri T 866 ABP, Daladala lenye namba T 574 AUP na Mitsubish lenye namba T 703 APH, iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Kimara Baruti Dar es Salaam. Ajali hiyo ilisababishwa na Roli lililokuwa likitokea Kimara kuja mjini baada ya kufeli breki na kuvuka upande wa pili wa barabara hiyo na kukutana uso kwa uso na magari mawili, Roli lililokuwa likielekea Morogoro huku likiwa na mizigo pamoja na Daladala lililokuwa na abiria likielekea Kimara ambapo imedaiwa kuwa dereva wa daladala hilo, alifariki papo hapo.
Raia wa maeneo hayo wakishuhudia ajali hiyo, ambapo kijana mmoja alipata kisago na kutiwa chini ya ulinzi wa Polisi wakati alipomchomolea fedha marehemu na kujaribu kutimka nazo na kuishia mikononi mwa polisi.
No comments:
Post a Comment