Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu hali halisi ya mgao wa umeme unaoendelea nchini, ambao unasababishwa na kuzidi kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa la Mtera ambapo hupungua sentimita tatu kila siku. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Badra Masoud.
HII SI COMMEDY LA HASHA ILIBIDI IWE HIVI.
HII SI COMMEDY LA HASHA ILIBIDI IWE HIVI.
Waandishi wa Habari, wakiigiza kuzungumza na waandishi wa habari kama viongozi wahusika wa Shirika la Umeme Tanesco, baada ya wahusika kuchelewa kuanza mkutano huo na waandishi wa habari leo asubuhi. Mkutano huo ulitakiwa kuanza saa tatu na nusu asubuhi lakini baada ya kufika waandishi wa habari muda ulisogezwa mbele na kuwaahidi waandishi kuwa ungeanza saa nne na nusu lakini hadi wanacommedy hawa wanaamua 'kubai taimu' kwa kuwachekesha waandishi ili muda usonge ilikuwa ni saa tano na robo, je namna hii masosi wasiojali muda wa wanahabari mwisho wa siku waandishi watachoka na kuamua kuondoka mahala hapo na pindi mtakapojisikia kunza mkutano wenu mtahutubia viti.
No comments:
Post a Comment