Habari za Punde

*WANAFUNZI WA MANZESE SEKONDARI WAFUNGA BARABARA LEO KUSHINIKIZA UZOAJI TAKA

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Manzese ya jijini Dar es Salaam, wakishangilia baada ya kufanikiwa kufunga barabara ya Tandale kwa kuweka takataka katikati ya barabara, baada ya kuziondoa katika eneo lao la shule kutokana na kukaa eneo hilo kwa muda wa siku tano bila kuondolewa. Wanafunzi hao walichukua hatua hiyo ya kuziondoa taka hizo baada ya kutozolewa kwa muda muafaka, hali ya kuwa wananchi wa maeneo hayo hutozwa Sh 1,500 kila mmoja kwa wiki kwa ajili ya uzoaji taka.
Hili si dampo la takataka, bali ni barabara ya Tandale eneo la Shule ya Sekondari Manzese, wanafunzi wakibeba mifuko ya takataka kuweka katikati ya barabara baada ya kuziondoa eneo la shule yao kutokana na harufu mbaya inayowakera wawapo madarasani. Wanafunzi hao walichukua hatua hiyo ya kuziondoa taka hizo leo, baada ya kukaa eneo hilo kwa siku tano, na kuamua kufunga barabara kwa kutumia taka hizo.
Hili si Dampo la takataka, ila ni barabara ya Tandale eneo la Shule ya Sekondari Manzese, ikiwa imetapakaa takataka zilizosambazwa na wanafunzi wa Shule hiyo baada ya kuziondoa eneo la shule yao kutokana na harufu mbaya inayowakera wawapo madarasani. Wanafunzi hao walichukua hatua hiyo ya kuziondoa taka hizo jana baada ya kukaa eneo hilo kwa siku tano, hali ya kuwa wananchi wa maeneo hayo hutozwa kiasi cha Sh. 1,500 kila mmoja kwa wiki kwa ajili ya uzoaji taka hizo.
Dereva wa daladala lililozuiliwa akijaribu kuondoa taka hizo chini ya gari ili aweze kupita eneo hilo.
Wanafunzi hao wakizidi kurundika taka katikati ya Barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.