Habari za Punde

*BONANZA LA NGUMI KUANZA DAR MWISHONI MWA MWEZI HUU


BONANZA la kwanza la aina yake la mchezo wa ngumi hapa nchini limepangwa kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kwenye viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Green Hills Tanzania Investment, George Andrew, alisema kuwa madhumuni ya bonanza hilo ni kuhamasisha vijana ili kujiunga na ngumi za kuliopwa au ridhaa na kuinua kiwango cha mchezo huo hapa nchini.

Andrew ambaye ni bondia wa zamani wa ngumi za ridhaa na kulipwa alisema kuwa wameamua kulifanya bonanza hilo ili kwenda tofauti na mabonanza mbali mbali ya mchezo wa soka, kikapu, netiboli na mchezo wa mpira wa wavu.

Alisema kuwa ni kawaida kwa Tanzania au wakazi wa miji mikubwa kuwa na matamasha ya michezo hiyo na kuachana na ngumi, jambo ambalo yeye kama bondia ameona ni bora kuweka historia kwa kufanya bonanza hilo.

“Lengo ni kuhamasisha mchezo wa ngumi hapa nchini bila kujali ni ngumi za ridhaa au za kulipwa, mimi ni bondia niliyepitia aina zote za ngumi hizo na kuona faida yake,
nimeweza kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kiataifa, naomba wadhamini na wadau wa mchezo wa ngumi watuunge mkono katika suala hili,” alisema Andrew.

Alisema kuwa mabondia wa zamana kama Anthony Mwang’onda, Benjamini Mwangata, Haji Matumla, Irag Hudu, Hamis Bwela, Lucas Msomba na Makoye Isangura, Koba Kimanga na Joseph Marwa.
Alifafanua kuwa siku hiyo, kutakuwa na lingo mbili, ambazo mabondia wa zamani na wa sasa watapigana kwa raundi mbili mbili kuanzia asubuhi mpaka jioni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.