Habari za Punde

*BONANZA LA WAANDISHI NA AIRTEL LAFANA

Mchezaji wa timu ya Global Publishers, akijiandaa kupiga shuti langoni mwa TBC wakati wa mchezo wao katika Tamasha la Bonanza la Waandishi wa Habari lililofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Posta Kijitonyama Dar es Salaam jana. Bonanza hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu za mkononi, Airtel.
Wachezaji wa timu za TBC na Global Publishers, wakichuana katika mchezo wa Netiboli.
Muda ulifikia wa kuanza kujisevia makulaji hapa kila mmoja akijihudumia na Plate yake.
Hawa nao sijui hata walikuwa wakishughulika na nini anga hizi wakati wenzao walikuwa katika foleni ya msosi wao wako bize na haya mananiliu. Hata hivyo (kushoto) ni John Bukuku na mwadada huyu wa Mwananchi, wanaonekana walikuwa wakichakachua 'Bips' za timu ya Taswa ili kuzitumia katika michezo hiyo na timu ya Mwananchi.
Hapa kila mmoja akiwa bize kujipatia msosi na kinywaji...
Eeeh! hapa ni msosi tu kwanza shibe mengine yanafuata.....
Wengine hata msosi hawakuwa na habari nao ila ni Biere tu kwenda mbele.....
"Heee! we acha kwanza nitafune nimejaza sana mdomoni usinipige picha bwaaaaanaaaa"
Huyu jamaa sijui alitumia sahani hizi zote ama la, kwani hapa anaonekana alikuwa ameshiba kupita kiasi na sahani hizi zote zikiwa pembeni yake na akiwa eneo hilo peke yake.......
Wengine waliamua kuwa Lonly hawakupenda bughudha, mdada huyu wa Redio Uhuru, Samirah Kiango, akiwa amepozi peke yake chini ya Tent akitafakari mambo yake....
Pombe siyo chai, ikikolea waweza kufanya lolote usilolitarajia, na hata ukijaelezwa baadaye unaweza kukataa, huyu ni mwandishi wa gazeti la Nipashe, Makore, akisakata rhumba na mnenguaji wa Msondo, Mama Nzawisa. wakiwa jukwaani, huku akijaribu kumsogeza ili wawe ziro distance.
Hapa ni waandishi wakijichanganya kusakata rhumba la Msondo kwa pamoja.
Eeeh! kila mmoja akijaribu kutoa staili yake ilimradi tu ni burudani katika Tamasha hilo.
Hapa dansi limekolea mwanawane, (kutoka kushoto) ni Crala wa Mwananchi, Timzoo wa Bingwa, Kambi wa Mtanzania na Gadiosa wa Nipashe, wakisebeneka na miondoko ya Msondo kwa pamoja.
"Hapo, Hapo sasa Hapo, Hapo sasa, mimi sisemi sikia mwenyewe"
Kila mmoja na asili yake, na Hobie yake, wengine wanapata burudani kwa kucheza dansi lakini jamaa huyu, James Range wa Star Tv, yeye burudani ni Biere tu.
Baadhi ya Wanamuziki waliokuwapo katika tamasha hilo, kutoka (kushoto) ni Hassan Moshi wa Msondo, Charls Baba wa Twanga na Kalala Junior wa Fm.Sufianimafoto akionyesha umahiri wa kuondoka na miondoko ya Msondo, baada ya kutangazwa kushinda na kuchukua kikombe kwa upande wa dansi kutokana na kutojitokeza washindani wengine, "ushindi wa kiulaiiini"
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari, wakimpongeza Sufianimafoto, baada kushinda na kutangazwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.