Mtaalamu wa Mambo ya kale katika chuo kikuu cha Colorado Denver, Dr. Charles Musiba, akimpa maelezo, Rais Jakaya Kikwete, kuhusu nyayo za binadamu wa kale aliyeishi zaidi ya miaka Milioni mia tatu, zilizopo Laetoli, kijiji cha Enduleni,Wilaya ya Ngorongoro. Nyayo hizo zilifukuliwa hivi karibuni kwa maelekezo ya Rais aliyeshauri wataalamu hao kuzifukua na kuzihifadhi ili watafiti na watalii wa ndani na nje ya nchi waweze kuziona na kuendelea na utafiti wa kisayansi. Nyayo hizo ziligunduliwa na mtafiti wa mambo ya Kale Dr. Mary Leakey huko Laetoli mwaka 1978 na kufukiwa ili zisiharibiwe na mmomonyoko wa ardhi. Picha na Freddy Maro
2,665 CBE wahitimu ngazi mbalimbali kampasi ya Dar ,Wananchi wachangamkia
Shahada za Uzamili mtandaoni za CBE
-
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeahidi kuendelea kukiwezesha Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),
ili kiwe chuo bora kituo cha umahiri kwa nchi za Afrika Masha...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment