Habari za Punde

*BONGOFLEVA FC YAIADHIBU BONGOMUVI FC 2-0

Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Bongofleva Fc, H-Baba, kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu hiyo na Bongomuvi Fc, uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Bongofleva Fc ilishinda mabao 2-0. picha zote na mtandao wa Jiachie
Kikosi cha timu ya Bongo Fleva.

TIMU ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Fc, leo jioni imeweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya wapinzania wao Bongomuvi Fc, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hizo baada ya kutambina kwa siku kadhaa huku kila timu ikitamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo uliokuwa maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasaidia waathirika wa mabomu wa Gongolamboto.


Mabao ya ushindi ya timu ya Bongo Fleva yalitiwa kimiani na Msanii H-Baba.

Kikosi cha timu ya Bongomuvi Fc.
Mwigizaji wa filamu, Ray 'Puuumbaaaavuuuuuu', akiambaa na mpira wakati wa mchezo huo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja, akitoa burudani jukwaani kabla ya kuanza kwa mtanange huo.
Mashabiki nao hawakukosekana katika mpambano huo.
Mchekeshaji Stive Nyerere, akiingia uwanjani kwa mkwara huku akiwa amezungukwa na wapambe.
Hata mchezo huu pia ulikuwa na vibweka vya aina yake ikiwa ni pamoja na wataalamu wa benchi za ufundi, hawa ni wasanii wakiingia uwanjani kwa mkwara wa ndumba, lakini wapi walilowa kwa goli mbili bila pamoja na mkwara wote huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, C-Pwaa, akitoa burudani jukwaani.
Mtangazi wa Redio Clouds, Millard Ayo (katikati) akikatiza mitaa ya ndani ya uwanja huo kusaka vimbwanga.
Baadhi ya wasanii walihudhulia.











No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.