Na Sufianimafoto Reporter, jijini
KOCHA Mkuu wa timu ya Vijana chini ya umri wa miaka 23, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, leo ametaja kikosi chake kitakachoanza kambi jumamosi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Fainali za kufuzu kucheza mashindano ya ‘Olympic’ yanayotarajia kufanyika mwakani, nchini Uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, ofisa habari wa Shirikisho hilo, Boniface Wambura, alisema kuwa timu hiyo itaanza kambi siku ya jumamosi ikiwa ni maalum pia kwa maandalizi ya mchezo wa kwanza na timu ya Taifa ya Vijana ya Cameroon, utakaochezwa Yaounde Machi 26.
Aidha alisema kuwa kabla ya mchezo huo timu hiyo inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu zitakazopatikana hapo baadaye kati ya Machi 12, 13 na 19 au 20 mwaka huu.
Kikosi hicho cha viajana chini ya umri wa miaka 23, kinatarajia kuondoka nchini Machi 22 kuelekea Yaunde kwa ajili ya mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa michuano ya Olympic.
ORODHA YA WACHEZAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA TIMU HIYO.
GOAL KEEPERS:-
1:- Saleh Malande –TSA
2:- Daudi Gabriel- Azam Fc
3:- Shaban Kado- Mtibwa Sugar
RIGHT AND LEFT BACKS:-
1:- Salum Telela-Yanga Fc
2:- Hassan Kessy- Mtibwa Sugar
3:- Issa Rashid- Mtibwa Sugar
CENTRE DEFENDERS:-
1:- Zahoro Pazi- African Lyon
2:- Mbwana Hamis- Simba Fc
3:- Louis Tumba- Azam Fc
4:- Omary Mtaki- Azam Fc
5:- Babu Ally- Moran Fc
MID FILDERS:-
1:- Godfrey Innocent- Simba Fc
2:- Ibrahim Juma-Azam Fc
3:- Samwel Ngasa- African Lyon
4:- Himid Mao- Azam Fc
5:- Seme Omega- Yanga Fc
6:- Frank Damayo- JKT Ruvu
7:- Salum Abubakar- Azam Fc
WING MID FILDERS:-
1:- Jamal Mnyate- Azam Fc
2:- Edward Shija- Simba Fc
3:- Cosmas Freddy- Azam Fc
STRIKER
1:- Benedict Ngasa- Moro United
2:- Atupele Green- Yanga Fc
3:- Mbwana Samatta- Simba Fc
4:- Thomas Ulimwengu- TSA
No comments:
Post a Comment