Habari za Punde

*MADJ's WAANZISHA CHAMA CHAO DAR

Na Sufianimafoto, jijini
MADJ’s wanaofanya shughuli za kupiga muziki katika sherehe mbalimbali, ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, wameanzisha Chama cha Madj’s, kwa ajili ya kusaidiana na kupiga hatu katika kufanya kazi zao kimataifa zaidi.

Akizungumza na Sufianimafoto, Mkurugenzi wa Chama hicho cha Madj’s ‘DJ’s Association’, Amri Dauda ‘Dj Tege’, alisema kuwa wameamua kuanzisha chama hicho ili kuwawezesha Madj’s, kuweza kupiga hatua zaidi kimaisha, kuboresha shughuli za madjs pamoja na kufanya kazi kwa kutambulika.

Aidha alisema kuwa tayari wamekwisha kamilisha taratibu zote za usajiri katika Baraza la Sanaa BASATA pamoja na COSOTA, ili kupewa haki zote za kufanya shughuli hizo kihalali na kulipia gharama za kodi za chama hicho za kila mwaka.

“Tayari tumeshasajiri Chama chetu na kupewa taratibu zote kisheria, naamini kuanzia sasa tunauwezo wa kufanya kazi popote bila wasiwasi na mpaka sasa chama chetu tayari kina jumla ya wanachama 24 halali walioishalipia ada zao za kiingilio” alisema Dauda

Pia alizitaja gharama za kujisajiri katika Chama hicho kuwa Mwanachama anapaswa kulipia Sh. 10,000 pindi anapojiunga na Sh. 10,000 kila mwezi ambayo inaingia katika akaunti ya chama na baadaye kuanzisha miradi itakayosimamiwa na chama hicho.

WANACHAMA WALIOJIUNGA NA CHAMA HICHO MPAKA SASA

1:- Amri Dauda
2:- Francis Bernald
3:- Shukuru Malewa
4:- Swed Hassan
5:- Haji Hassan
6:- Seif Ally
7:- Lous Trezzo
8:- Hussein Idd
9:- Khalfan Abdallah
10:- Hamad Abdallah
11:- Seif Iddy
12:- Ernest Lightson
13:- Khalid Ibrahim
14:- Said Hassan
15:- Deodatus Joseph
16:- Emmanuel Mkonyoka
17:- Fidelis Mkama
18:- Cuthbert Valentine
19:- Michael Katambi
20:- Hassan Nyengele
21:- Godson Mbeikya
22:- George Juma
23:- Denis Elbarick
24:- Muhidin Sufiani


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.