Habari za Punde

*SIMBA YAWAHADHIBU WADOGO ZAO AFRICAN LYON 3-0

Wachezaji wa Simba na African Lyon, wakichuana kuwania mpira wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo jioni. SImba imeshinda mabao 3-0. Wafungaji wa mabao hayo ni Amri Kiemba, aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 5 ya mchezo na Mbwana Samatta, aliyefunga bao la pili Dakika ya 46 na 82. Kwa ushindi huo sasa Simba imefikisha jumla ya Pointi 30 ikiwa nyuma kwa pointi 1 na watani wao Yanga ambao wanapointi 31. Nafasi ya tatu wapo Azam Fc wenye pointi 26 sawa na Mtibwa Sugar ambao nao wanapointi 26 wakiwa katika nafasi ya nne, wakiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, nafasi ya nne wapo Kagera Sugar wakiwa na Pointi 22.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.