Habari za Punde

*TBL YAZINDUZ VIWANJA VYA NETIBOLI, KIKAPU NA WAVU MKOANI KILIMANJARO

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Christopher Mutamakaya (katikati), akiongozana na Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi, Profesa Faustine Bee (kulia) pamoja na Meneja wa TBL Kanda ya Kaskazini Mashariki, Kasiro Msangi, wakati wakikagua Uwanja wa Chuo hicho, uliokarabatiwa na Kampuni ya Bia TBL na kuukabidhi kwa uongozi wa chuo leo hicho leo. Uwanja huo umeanza kutatumika leo kwa mbio za Kilimanjaro Marathon.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Christopher Mutamakaya, akijiandaa kurusha mpira golini wakati wa uzinduzi wa uwanja wa kikapu uliojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, wakati wa shamrashamra za uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro zinazodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, TBL . Katika uzinduzi huo TBL pia ilikadhi viwanja vya netiboli na wavu kwa uongozi wa chuo hicho leo.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.