Habari za Punde

*THT YAZINDUA MRADI WA 'THEATRE IN EDUCATION' KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUTOA ELIMU YA MALARIA

Mratibu wa Elimu ya Afya, Maji na Mazingira kutoka Wizara ya Elimu, Teresia Kuiwite, akipiga ngoma kuashiria uzinduzi wa Mradi wa kupambana na Malaria wa ‘Theatre in Education’, utakaotoa mafunzo mbalimbali ya kujikinga na ugonjwa huo katika shule za sekondari nchini. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Wasanii wa kundi la THT, wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo leo.

Na Sufianimafoto, jijini
TANZANIA House Of Talent (THT), leo imezindua mradi wake wa kupambana na Malaria uitwao ‘Theatre in Education’ utakaotoa mafunzo mbalimbali ya kujikinga na ugonjwa huo katika shule za sekondari nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es salaam leo, urugenzi wa mradi huo, Sadaka Gandi alisema THT itakuwa na ujumbe wa wasanii 14 watakaozunguka nchi nzima kutoa elimu hiyo kupitia sanaa.

Sadaka alisema mwaka jana THT kwa kushirikiana na Malaria No More walianzisha kampeni ya kitaifa ya mawasiliano kwa mabadiliko ya tabia ya nchi Tanzania, kwa lengo la kupambana na Malaria na kuzuia vifo visivyokuwa vya lazima hadi kufikia mwaka 2015.

Akizindua mradi huo, Mratibu wa Elimu ya Afya, Maji na Mazingira kutoka Wizara ya Elimu, Teresia Kuiwite alizitaka taasisi nyingine kujitokeza kwa wingi kuungana na serikali kutokomeza ugonjwa huo nchini.


Uzinduzi wa mradi huo ulipambwa na burudani kutoka kwa mabalozi 14 wa THT na kuhudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari za Jitegemee, Chang’ombe, DYCC, Benjamin Mkapa na Kibasila.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.