Habari za Punde

*WANAFUNZI WA IFM WAGOMA KUINGIA MADARASANI

Mmoja kati ya viongozi wa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, aliyetambulika kwa jina moja la Moses, akiwafafanulia jambo wanafunzi wenzake wakati walipogoma kuingia madarasani leo asubuhi, wakidai haki zao.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wakiwa wamekusanyika nje ya madarasa, baada ya kugoma kuingia madarasani kwa kile walichodai kushinikiza uongozi wa Chuo hicho kumwondoa mwenyekiti wa chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kudai baadhi ya wanafunzi waliozuiliwa kufanya mitihani kwa sababu ya kutomalizia ada, waruhusiwe kufanya mitihani hiyo, inayoendelea chuoni hapo.

Na Joseph Ishengoma-
MAELEZO, Dar es Salaam

Wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar Es Salaam leo wameanza mgomo wa amani kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kukubaliana na mapendekezo yao katika utoaji wa vitambulishio vya kuingilia katika vyumba vya mitihani.
Aidha wanafunzi hao wanalalamikia kutopatiwa matokeo ya mitihani yao ya majaribio (course work), nakuruhusiwa kufanya mitihani hata wale ambao bado hawajamalizia ada zao.
Waziri wa Mikopo wa IFM Bwana Juma George amesema kuwa, “tumekusanyika hapa baada ya njia mbadala za kutatua matatizo yetu hapa chuoni kushindikana.”
Bwana George amesema, “Badhi yetu tumelipa ada inayotakiwa, lakini hatukupata vitambulisho, baadhi wamepata na wengine hawana uwezekano kabisa wa kulipa ada.” Kwa mujibu wa kiongozi huyo, zoezi la utoaji wa vitambulisho lililoanza tangu Jumatano iliyopita limegubikwa na mizengwe mingi kutoka kwa uongozi wa chuo na kusababisha baadhi yao kuzirai katika mistari wakati wakisubilia vitambulisho hivyo.
Wanafunzi wanaotakiwa kupatiwa vitambulisho ni wale waliomaliza ulipaji wa ada yao , kuhudhuria masomo yao darasani kwa asilimia 75 na kumaliza
Mgomo huo umeanza siku ambayo chuo hicho kilitarajiwa kuanza mitihani yake, hata hivyo Makamu Mkuu wa chuo Prof . Godwin Njema amesogeza mbele wiki moja hadi Jumatatu ijayo mitihani hiyo.
Akiongea mbele ya wanafunzi waliokusanyika katika viwanja vya chuo hicho, Waziri wa Elimu wa serikali ya wanafunzi Bwana George Anthony amesema, “tumegomea urasimu uliopo chuoni hapa sio mitihani. Mgomo wetu ni wa amani, hakuna uvunjifu wa mali , matusi wala kebehi.”
Wanachuo hao wanautaka uongozi wa chuo kuwaruhusu wanafunzi wote walioko chuoni hapo ambao hawajamaliza kulipa ada kufanya mitihani yao bila masharti wakinukuu agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete kuwa “hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kufanya mtihani kutokana na kukosa ada.”
“Tumetoa mapendekezo ya aina mbalimbali kwa uongozi wa chuo kuhusiana na tatizo hili, lakini hautaki kutusikiliza. Badala yake baadhi ya watumishi wa chuo wamekuwa wakitoa lugha za kebehi, matusi na maneno ya kashfa tunapofuatilia tatizo hili.”
Akiongea mbele ya wanafunzi hao, Prof. Njema amesema, “suala la vitambulisho litaendelea kushughulikiwa na ifikapo Jumatatu ijayo terehe 5/3/2011 kila mwanafunzi anayestahili atakuwa na kitambulisho chake.”
“Hata kama mtu asingekuwa na kitambulisho, chuo kinautaratibu maalum wa kutoa namba za mitihani kwa wanafunzi wote waliotimiza masharti. Wanafunzi nyote mtawanyike kuelekea madarasani kwenu. Kama mmekubaliana nami nikielekea ofisini nanyi nendeni darasani kujiandalia mitihani,” amesema huku wanafunzi wakipiga kelele za kupinga maelezo yake.
Kuhusu ada amesema, “suala la ada kwa mwanafunzi inabidi lishughulikiwe na mwanafunzi mwenyewe. Mmapoamua kugoma kwasababu ya ada hii ilitakiwa kuwa hatua ya mwisho kabisa.”
Mku huyo wa chuo ameeleza mkusanyiko huo kuwa matatizo yao yanatatuliwa na amewataka watume wawakilishi wacheche wakujadiliana nao, kauli iliyopingwa na umati wa wanafunzi huku ukimtaka kujibu maswali yao hadharani bilal kuita kundi dogo la wanafunzi.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.