Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akiwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati alipokutana nao leo Chuoni hapo kwa ajili ya kusikiliza malalamiko yao. Wanafunzi hao walitawanywa na askari kwa kutumia mabomu baada ya kuanza kuwashambulia askari kwa mawe na chupa za maji kutokana na hasira za kutopewa majibu yanayoridhisha kuhusu madai yao, baada ya mkutano huo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akiondoka eneo la mkutano akiwa chini ya usimamizi wa Polisi baada ya kumaliza kuwahutubia wanafunzi hao.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akiondoka eneo la mkutano akiwa chini ya usimamizi wa Polisi baada ya kumaliza kuwahutubia wanafunzi hao.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakimbeba mwenzao kumkimbiza hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa na Bomu la machozi baada ya askari wa kutuliza ghasi (FFU) kuanza kufyatua mabomu ili kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wakirusha mawe na chupa za maji baada ya mkutano huo. Mwanafunzi huyo akiwa na jeraha mgongoni baada ya kupigwa na bomu la machozi.
Wanafunzi wakimuokoa mwenzao baada ya mabomu hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakijaribu kukimbia bila mwelekeo baada ya Askari wa kutuliza ghasia (FFU) kuanza kufyatua mabomu chuoni hapoa.
" Duh! Watoto wananitoa jasho hawa sijui nifanyeje hapaaaa!"
Wanafunzi hao wakipanda juu ya paa kuwahi nafasi kabla ya waziri kuwasili eneo hilo.
Sehemu ya umati wa wanafunzi hao wakiwa eneo la mkutano.
"Hapa hadi kielewekw" Jamaa akiwa na bango lenye Ujumbe wa Waziri, wakati wakimsubiri awasili Chuoni hapo.
Wanafunzi wakitoa huduma ya kwanza kwa mwenzao mwanadada aliyeanguka ghafla na kupoteza fahamu kutokana na mabomu yaliyorindima Chuoni hapo baada ya mkutano na Waziri wa Elimu.
No comments:
Post a Comment