MKUU wa wilaya ya Ngorongoro, Elius Lali, amesema kuwa msongamano wa magari ya watu waliokwenda kunywa dawa ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile, unatarajia kupungua Machi 17 mwaka huu.
Wawa, alisema hayo leo wakati akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya simu ambapo alibainisha kwamba tayari mageti yote ya barabara ya Mto wa Mbu na lile la barabara inayotokea Musoma kuingia Loliondo yamekwisha kufungwa ili kuzuia magari yasiendelee kuingia katika Kijiji cha Samunge.
“Tumeweka askari wa kutosha Ngorongoro tumekwisha funga mageti ya kuingilia na magari hayaruhusiwi tena kuingia kwa kipindi hiki, hadi hapo yatakapokuwa yamepungua, kwa hiyo naamini hata huko Mto wa Mbu Monduli kutakuwa na mageti tayari,” alisema Wawa Lali
Hata hivyo kutokana na msongamano mkubwa uliokuwa ukielekea nyumbani kwa Mchungaji Mwasapila kufikia takribani kilomita 20, tayari umeanza kupungua baada ya magari mengi kuanza kutoka.
“Msongamano umepungua hivi sasa zimebakia foleni za magari yaliyopo mkwenye mistari tofauti na mwanzo ambapo magari mengi yalikuwa yametapakaa pembeni na kusababisha usumbufu zaidi kutokana na aina ya njia za vijijini,” alisema DC
Kutokana na hatua hiyo hivi sasa katika eneo la Mto wa Mbu kumekuwa na ongezeko la watu wengi ambao wameshindwa kuingia ndani ya barabara ya vumbi kuelekea Kijiji cha Babu Mchungaji Mwasapila ili kunywa dawa.
Hata hivyo taarifa zinasema kwamba baadhi ya watu wengine wamelazimika kutumia njia za panya ili kufika kwa Mchungaji Mwasapila.
No comments:
Post a Comment