Habari za Punde

*DSTV YATOA SOMO KWA STAR TV

Mkurugenzi wa Super Sport, Sifiso Mbambo, (kulia) akitoa maelezo ya jinsi gari hilo la kurushia matangazo linavyofanya kazi wakati waandishi wa habari na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, walipotembelea katika gari hilo.

Na Sufianimafoto Reporter, jijini

GARI la kurushia matangazo la Super Sport la nchini Zambia kupitia DSTV, imewasili nchini na kutoa somo wafanyakazi wa Star Tv ikiwa ni sehemu ya kuwafundisha na kuwapa uzoefu zaidi ili kuboresha matangazo wanayorusha ya Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara kutoka Analogi na kufikia hatua ya kidigito.

Super Sport waliowasili nchini hivi karibuni wakitokea nchi Zambia walifika maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo kadhaa kwa Star Tv kupitia mchezo wa Ligi Kuu wa Watani wa jadi Yanga na Simba uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mchezo huo ulikuwa ukionyeshwa live kupitia DSTV.

Akizungumza na gazeti hili ‘Unit Super Visor’ wa gari la kurushia matangazo la DSTV, Trevor Tachiona, alisema kuwa mchezo huo wa Yanga na Simba ulikuwa ukitazamwa na jumla ya nchi 32 kupitia Super Sport.

Aidha alisema kuwa kutokana na ubora wa timu hizo zenye historia nzuri katika Afrika, ndiyo hasa sababu kubwa iliyofanya kuacha kurusha michezo ya Ligi kuu ya Zambi iliyokuwa ikiendelea kwa siku hizo walizokuwa nchini na kuja kurusha mchezo huo ili kuwafanya Star Tv kuweza kuwa na uzoefu zaidi na kuboresha kazi zao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.