Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, Jerry Slaa, akikata utepe kuzindua rasmi duka la Sanaa la Ujamaa Art Gallery na Mkurugenzi wa Duka hilo, Lorna Mashiba (katikati) wakati wa uzinduzi uliofanyika jana jioni maeneo lilipo duka hilo Mbuyuni. Kulia ni mke wa Jerry, Anna Slaa na (kushoto) ni Shama Jaffer.
Mstahiki Meya wa Ilala Jerry Slaa na mkewe Anna Slaa (kushoto) wakionyeshwa baadhi ya picha zilizochorwa na wasanii wa nchini, na Mkurugenzi wa duka Ujamaa Art Gallery, Lona Mashiba (wapili kulia) na 'Curator Artist' , Shama Jaffer, zilizowekwa katika duka hilo wakati wa uzinduzi

DUKA la Ujamaa Art Gallery, lililozinduliwa jijini Dar es salaam jana jioni kwa lengo la kuendeleza, kusimamia na kuuza kazi za wasanii wa uchoraji nchini limepanga kutoa mauzo yake ya wiki moja baada ya uzinduzi huo ili kuwasaidia waathirika wa mabomu wa Gongolamboto.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Lorna Mashiba, ambaye ni Mkurugenzi, alisema kuwa mauzo yatakayopatikana ndani ya wiki ya kwanza baada ya kuzinduliwa, yatapelekwa kuwasaidia waathirika wa mabomu.
Aidha Duka hilo lililozinduliwa kwa lengo la kuwasaidia wasanii wa Sanaa ya uichoraji, litakuwa likisambaza kazi za wasanii hao ndani na nje ya nchi ili kuweza kutangaza zaidi kazi za wasanii wa nyumbani ili kufikia hatua ya kimataifa.
“Tumeamua kufungua kampuni hii ili tuwawezeshe wasanii wa nyumbani wa Sanaa ya uchoraji, waweze kujitangaza kimataifa na kazi zao ziweze kutambulika kimataifa” alisema Lorna.
Lorna, alisema kuwa kampuni hiyo itakuwa ikipokea kazi za wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam na kuziweka katika ofisi ya duka hilo ili wateja wasioweza kuwafikia wasanii hao iwe rahisi kwao kufika katika ofisi hizo na kupata huduma hiyo kwa urahisi.
Akizindua Duka hilo, Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Slaa, aliwashukuru wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuanzisha utaratibu huo na kusema kuwa utaongeza ajira kwa vijana wengi na kuongeza vivutio vya utalii ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Aidha aliwashukuru pia kwa kujitolea mapato ya wiki nzima baada ya uzinduzi huo ili kuwachangia waathirika wa mabomu wa Kata yake ya Gongolamboto na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuwasaidia waathirika hao ambao miongoni mwao bado wamelazwa wakiendelea kpata matibabu.
“Nawashukuru wamiliki wa kampuni hii kwa kujitolea kusimamia na kuuza kazi za wasanii pamoja na kuwachangia waathirika wa Kata yangu, kwani tatizo hili ni la kitaifa na limemgusa kila mtu na pia jiji letu sasa litakuwa na moja ya kivutio cha utalii kwa wageni watakaokuwa wakiingia na kutoka nchini iwapo wahusika wataweza kujitangaza zaidi. Alisema Slaa

Wageni waalikwa wakiangalia baadhi ya picha zilizochorwa na kuwekwa katika duka hilo baada ya uzinduzi rasmi.
No comments:
Post a Comment