Habari za Punde

*NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NYALANDU ATEMBELEA SHIRIKA LA VIWANGO LEO

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Lazaro Nyalandu (kushoto)akitembelea maabara na maeneo mbali mbali katika ziara yake ya kutembelea Shirika la Viwango nchini TBS, leo.Picha na Othman Michuzi

Na Mwandishi Wetu, Jijini

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, amelitaka Shirika la Viwango Nchini (TBS) kuongeza juhudi katika kusimamia ubora wa bidhaa nchini ili kuwapa watumiaji thamani halisi ya fedha wanazotumia katika kununua bidhaa hizo.

Nyalandu ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kulitembelea Shirika la Viwango nchini TBS ambalo lipo chini ya Wizara yake.

“TBS mnalinda maisha ya watu, mnalinda mali zao, fanyeni kazi zenu kwa umakini mkubwa, bila woga, serikali haitawaingilia na badala yake, itawasimamia na kuwawezesha ili mtimize vyema majukumu yenu” alisema Naibu Waziri

Akimkaribisha Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw Charles Ikerege amesema, TBS imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kusimamia ubora wa bidhaa nchini licha ya uwezo mdogo wa kifedha ilionao na kuiomba serikali kuongeza fungu la fedha ili kulipa shirika hilo uwezo zaidi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.